Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2017

KOCHA TAIFA STARS ATANGAZA KIKOSI CHA MAANGAMIZI

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachocheza michezo yake ya kimataifa inayokuja. Kikosi hicho kimejumuisha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi pamoja na wanaocheza ligi ya ndani. Makipa Aishi Manula Peter Manyika Ramadhan Kabwili Mabeki Boniphas Maganga Abdi Banda Gadiel Michael  Kelvin Yondani Salim Mbonde Erasto Nyoni Adeyuni Salehe Viungo Himid Mao Hamis Abdallah Mzamiru Yassin Raphael Daud Simon Msuva Shiza Kichuya Ibrahim Ajib Morel Ergenes Abdul Hilal Hasan Washambuliaji Mbwana Ally Samatta Mbaraka Yusuph

DAKIKA 90 ZA SINTOFAHAMU NCHINI UINGEREZA

Ni dakika 90 za sintofahamu kwenye viwanja mbalimbali nchini Uingereza. Na hii ni kutokana na fomu pamoja uwezo wa timu hizo zinazomenyana wikiendi hii kushabihiana ukiachilia mbali usajili uliofanywa na baadhi ya timu hizo. 14:30 EAT - West Ham United vs Tottenham  Mapema kabisa vijana wa London watamenyan aikiwa ni West Ham United watawakaribisha Tottenham kwenye dimba la London Stadium. West Ham United imekuwa ikihangaikakutafuta matokeo mazuri tangu kuanza kwa msimu wa 2017/2018 na kufanikiwa junyakua pointi 4 tu kwenye mechi 5. Timu hiyo imefunga magoli 4 na kuruhusu 10 nyavuni mwake. Hiyo ni ishara ya safu mbovu ya ulinzi na safu butu ya aidha ushambuliaji au kiungo. Kwa kuwa kwa mchezaji mmoja mmoja wana uwezo basi tutegemee mabadiliko siku baada ya siku. Na vipi hiyo siku baada ya siku ikianza leo? Kwa upande wa Tottenham, ni timu bora iliyojiimarisha tangu msimu uliopita japokuwa hawakuanza msimu kama ilivyotegemewa na wengi ukichukulia kwamba hawajauza wachezaji w...